Habari za michezo

KISA ANGUKO LA SIMBA MSIMU HUU…AHMED ALLY AENDELEA KUTOA ‘MAHUBIRI YA FARAJA’ INSTAGRAM…AWASHUKIA WENYE CHUKI…

admin May 31, 2022 8:38 am


Meneja wa Habari na Mwasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amewashukia baadhi ya wadau wa Soka wanaotumia kipindi hiki kutaka kuvuruga utulivu na amani ndani ya klabu hiyo, kwa kigezo cha kupoteza mataji ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho ‘ASFC’.

Simba SC ilipoteza muelekeo wa kutetea taji la ‘ASFC’ Jumamosi (Mei 28) kwa kukubali kufungwa 1-0 na Young Africans, katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Ahmed Ally amewataka Mashabiki na Wanachama wa Simba SC kuhakikisha wanaendelea kuwa kitu kimoja kama ilivyokua kabla hawajapoteza Ubingwa.

Amesema wanaotumia kipindi hiki kupenyeza Chuki zao kwa kutoa maneno ya Kashfa na Kebehi, wanatakiwa kupuuzwa kwa hali zote, kwani Simba SC ina mipango yake kuelekea msimu ujao, baada ya kuanguka msimu huu.

Ahmed Ally ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kufikisha ujumbe huo kwa Mashabiki na Wanachama wa Simba SC kwa kuandika: Nipo imara na naendelea na mapambano

WAMOROCCO WASEPA NA MAKOMBE YOTE YA CAF MSIMU HUU…WYDAD WABEBA BILIONI 5 ZA UBINGWA…. UBORA WA YANGA MSIMU UWE KENGELE YA HATARI KWA SIMBA…WAACHE UBAHILI WA KUSAJILI…LA SIVYO JAHAZI LITAZAMA KABISA..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply