CAF

WAMOROCCO WASEPA NA MAKOMBE YOTE YA CAF MSIMU HUU…WYDAD WABEBA BILIONI 5 ZA UBINGWA….

admin May 31, 2022 8:34 am


Miamba ya Soka ya nchini Morocco Wydad Casablanca wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Klabu bingwa Afrika, baada ya kuwafunga mabingwa watetezi National Al Ahly ya Misri mabao 2 – 0.

Magoli ya dakika ya 15 na 48 yaliyofungwa na Zouhair El Moutaraji yameifanya Wydad kutwaa taji lake la 3 la michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Al Ahly waliokuwa wakitetea taji hilo, licha ya kushambulia muda mwingi katika mchezo huo lakini wameshindwa kufurukuta katika fainali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mohammed V Jijini Casablanca, Morocco

Ubingwa huo wa tatu kwa Wydad unawapa Dola 2,500,000 (Tsh. Bilioni 5.7) wakati Al Ahly wameambulia Dola 1,250,000 (Tsh. Bilioni 2.7) kwa kushika nafasi ya pili.

Kwa ushindi huo ni wazi kuwa Klabu za Soka za nchini Morocco zimetawala Soka la Afrika msimu huu baada ya RS Berkane kutwaa taji la kombe la Shirikisho barani Afrika majuma mawili yaliyopita.

FINALISSIMO NDANI YA SuperSport…WABABE KAMA WOTEE WA DUNIA KUKIWASHA… MZIGO WOTE HUU NDANI YA DStv…. KISA ANGUKO LA SIMBA MSIMU HUU…AHMED ALLY AENDELEA KUTOA ‘MAHUBIRI YA FARAJA’ INSTAGRAM…AWASHUKIA WENYE CHUKI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply