Home Azam FC AZAM FC WAMSHUSHIA LAWAMA MWAMUZI WA JANA…WADAI IMETOSHA…WAHOJI KWA NINI KILA SIKU...

AZAM FC WAMSHUSHIA LAWAMA MWAMUZI WA JANA…WADAI IMETOSHA…WAHOJI KWA NINI KILA SIKU WAO TU..?


Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino Azam FC Thabit Zakaria ‘Zakazakazi’ amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ kupitia kamati ya Waamuzi, kumfikiria Mwamuzi mwingine tofauti na Heri Sasii ambaye anadaiwa kuchezesha michezo muhimu na mikubwa kwa klabu hiyo.

‘Zakazakazi’ ametoa ombo hilo TFF, baada ya Mwamuzi huyo kuchezesha mchezo wa jana Jumatano (MEi 18), dhidi ya Simba SC kwenye Uwanja wa Azam Complex-Chamazi jijini Dar es salaam na timu hizo kuambulia matokeo ya 1-1.

‘Zakazakazi’ amesema Mwamuzi huyo kwa msimu huu amechezesha mchezo wao dhidi ya Young Africans kisha alipewa nafasi hiyo katika mchezo dhidi ya Simba SC na jana amerejea tena Dimbani kuchezesha mchezo dhidi Mabingwa hao wa Tanzania Bara.

“Tumechoka na Heri Sasii, kwani hakuna waamuzi wengine ? Tunaiomba bodi ya ligi isitupangie tena mwamuzi Heri Sassi”,

“Kwa nini michezo yetu yote dhidi ya Simba anachezesha Heri Sassii, mechi ya Round ya kwanza alichezesha Sassii, mechi yetu dhidi ya Yanga alichezesha Herri Sassi, mechi ya Round ya pili dhidi ya Simba kachezesha Sassiii,, kwani hakuna waamuzi wengine ?!” amehoji ‘Zakazakazi’

SOMA NA HII  BAADA YA DIRISHA LA USAJILI KUFUNGWA....MASTAA WA KICONGO WAJAZANA ZAIDI YANGA...TAKWIMU HIZI HAPA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here