Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA KANOUTE….SIMBA SC WAVUNJA UKIMYA KUHUSU YANAYOENDELEA JUU YAKE…

KUHUSU ISHU YA KANOUTE….SIMBA SC WAVUNJA UKIMYA KUHUSU YANAYOENDELEA JUU YAKE…

Habari za Simba

Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wameeleza kilichomfanya nyota wao Sadio Kanoute akosekane kwenye mchezo wa dabi dhidi ya Yanga SC pamoja na mechi nyingine zilizotangulia zikiwemo mbili dhidi ya Ihefu FC.

Akizungumza na waandishi wa habari , Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally, alisema, Kanoute alipata majeraha ya nyonga hivyo ataingia kambini leo na kisha kufanyiwa vipimo kujua kama anaweza kuendelea na mazoezi au la.

“Kanoute, anasumbuliwa na nyonga, atakutana na madaktari leo kujiridhisha kama yupo fiti ataanza mazoezi,” alisema Ahmed.

Ahmed alisema, mwingine ambaye alikuwa majeruhi ni golikipa namba moja Aishi Manula ambaye naye leo atawasili kambini na madaktari wataangalia, kama tatizo lake linaweza kupona lenyewe au atahitajika kufanyiwa upasuaji.

Kuhusu Agustine Okrah, Ahmed alisema alishapona siku nyingi, alianza mazoezi lakini hakuwa fiti kuanza dhidi ya Yanga hivyo anaendelea na mazoezi.

SOMA NA HII  MWISHO WA UBISHI GLOBAL FC V DStv LEO