Home Burudani HUYU HAPA STAA WA BONGO FLEVA ALIYEPEWA SHAVU NA SERGIO RAMOS WA...

HUYU HAPA STAA WA BONGO FLEVA ALIYEPEWA SHAVU NA SERGIO RAMOS WA PSG….

Ramos aposti wimbo wa Staa wa Bongo Fleva mavokali

Mchezaji wa Klabu ya Psg, Sergio Ramos, ametumia wimbo wa Commando wa msanii Bongo Fleva, Mavokali, kwenye ‘Insta Story’ yake.

Ramos, ameposti picha hiyo akiwa na wenzake Carlos Regli na Manuel Jara.

Wimbo wa Mavokali, Commando ulitoka rasmi 28 Sept 2022 na video ya ngoma hiyo ina zaidi ya watazamaji milioni 15 kwenye mtandao wa Youtube.

Hii ni mara nyingine tena staa mkubwa wa soka kupost wimbo wa staa wa kibongo, ambapo hivi karibuni Real Madrid walipost wimbo wa Rayvanny katika kumtakia kheri ya kuzaliw staa wake Karim Benzema.

SOMA NA HII  BAADA YA TIMU ZA TZ KUMSHINDWA ....IBENGE APATA SHAVU NONO LA KUINOA AL HILAL...APEWA MALENGO KAMA YA SIMBA...