Home Habari za michezo MASHINE MPYA YA KAZI YANGA KUTAMBULISHIWA ZNZ….ALLY KAMWE ATAJA ‘CODE’ YAKE…

MASHINE MPYA YA KAZI YANGA KUTAMBULISHIWA ZNZ….ALLY KAMWE ATAJA ‘CODE’ YAKE…

Habari za Yanga

Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans wameingia kambini leo Jumanne (Desemba 27) kuanza kujiwinda na mchezo wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Jamhuri utakaochezwa kwenye Uwanja Amaan, Zanzibar Jumapili (Desemba 31).

Young Africans imepangwa Kundi C na timu za Jamhuri na KVZ zote kutoka visiwani Zanzibar na Jamus kutoka Sudan Kusini.

Michezo yote ya Kombe la Mapinduzi itachezwa katika Uwanja wa Amaan na kesho Alhamis (Desemba 28) ndio ufunguzi kati ya Mandege dhidi Azam FC saa 10-00 jioni.

Ofisa Habari wa Young Africans, Ali Kamwe, amesema kuwa baada ya mapumziko mafupi waliyopewa wachezaji baada ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tabora United wamerudi kuanza kujiwinda na Kombe la Mapinduzi.

“Kikosi kimerejea kambini leo kuaza kujiwinda na michuano ya Kombe la Mapinduzi ambayo ni mashindano muhimu kwetu kutengeneza muunganiko wa kikosi chetu.

Lakini pia ni wakati wa kwenda kutambulisha nyota wapya tuliowasajili kwenye dirisha dogo la usajili na kwenye mchezo wetu wa kwanza tutatambulisha kifaa chetu kipya ambacho kimekuja kuongeza nguvu kikosini,” amesema Kamwe.

Katika hatua nyingine Kamwe amesema kikosi cha Young Africans kinatarajia kuanza safari kesho Alhamis (Desemba 28) kwenda Zanzibar kwa ajili ya michuano hiyo ambayo malengo yao ni kuhakikisha wanarudi nyumbani na kombe.

Mchezo wa pili Young Africans itacheza na Jamus FC, Januari 2 mwakani na mchezo wa mwisho kwenye makundi watacheza na KVZ Januari 4.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA KESHI NA SIMBA....MATAJIRI YANGA WAITANA 'FASTA' KUMALIZIA KAZI...