Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA SIMBA NA WAMOROCCO…MSUVA AWAFANYIA KITU MBAYA WYDAD…AANIKA SIRI ZAO...

KUELEKEA MECHI YA SIMBA NA WAMOROCCO…MSUVA AWAFANYIA KITU MBAYA WYDAD…AANIKA SIRI ZAO ZOTE..

Habari za Simba SC

Staa wa zamani wa Yanga, Simon Msuva ambaye aliwahi kucheza kwenye Ligi ya Morocco dhidi ya Wydad Casablanca alisema mara nyingi timu za Kaskazini zimekuwa na hesabu kubwa sana kwenye michezo yao wakiwa ugenini.

Anasema wamekuwa wakipoteza muda uwanjani na kutafuta sare hasa katika hatua kama hii. “Najua kwa kiasi fulani tabia ya timu za Kiarabu, ni wanjanja sana, huwa hawatumii nguvu kubwa ugenini, hucheza kwa kupoteza muda, ni muhimu kuwa na nidhamu ya mchezo dhidi yao, hilo Simba wanatakiwa kuliangalia kwa umakini,” alisema mshambuliaji huyo.

Msuva ambaye anacheza soka la kulipwa Saudi Arabia akiwa na Al-Qadsiah, aliichezea Wydad Casablanca 2020–2022, wapo wachezaji wa kikosi hicho ambao alikiwasha nao mwanzoni mwa msimu wa 2021–22 kwenye ligi ya Mabingwa Afrika kabla mgogoro wake na vigogo hao ambao baadae walibeba taji hilo.

Kwa upande wa Kocha wa Simba SC Roberto Oliveira ‘Robertinho’ alisema sasa wanakwenda kumaliza kazi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca.

“Tumekuwa na michezo mingi mizuri na mikubwa ambayo imetuweka kwenye kiwango chetu, bado tunatakiwa kupambana ili kuwa bora zaidi, ninafuraha na viwango vya wachezaji wangu, wamekuwa wakitoa kile ambacho kipo ndani ya uwezo wao na muda mwingine hufanya zaidi hilo ni jambo zuri,”

“Hatupaswi kubweteka na kuona kazi imemalizika baada ya kuifunga Yanga, kwetu kazi ndio imeanza kwa sababu kuna michezo mingi mbele yetu kwa sasa ni wakati wa kukabiliana na Wydad, tunajua kuwa hautakuwa mchezo mwepesi lakini lazima mtambue kuwa sisi ni Simba,” alisema kocha huyo.

SOMA NA HII  SIKU CHACHE BAADAYA SIMBA KUCHEZEA KICHAPO MORO....TFF WAFUNGA UWANJA....