Home Habari za michezo BAADA YA SIMBA KUKAZIWA NA NAMUNGO JANA….PABLO ASHINDWA KUJIZUIA..AWATAJA WALIO ZINGUA…

BAADA YA SIMBA KUKAZIWA NA NAMUNGO JANA….PABLO ASHINDWA KUJIZUIA..AWATAJA WALIO ZINGUA…


Kocha Mkuu Pablo Franco, ameweka wazi kuwa wamefanya makosa ya kiulinzi yaliyoifanya Namungo kupata mabao mepesi katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 katika Uwanja wa Ilulu.

Pablo amesema wao  kama timu kubwa inayopambania ubingwa hawatakiwi kufanya makosa kama yale ambayo yanazidi kuwaweka katika mazingira magumu.

Mbali na safu ya ulinzi kufanya makosa Pablo amesema pia hakuwa vizuri katika kumalizia nafasi tuwalizopata hasa kipindi cha kwanza.

“Kwa timu kubwa kufanya makosa ya kiulinzi kama vile haileti picha nzuri. Pia tumetengeneza nafasi ambazo hatukuzitumia vizuri.

“Tutarudi kuendelea kujipanga kwa mchezo unaofuata, bado hatujakata tamaa tutahakikisha tunapambana kupata alama tatu kwenye kila mechi,” amesema Pablo.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA REAL BAMAKO....NABI ATUMA SALAMU NZITO KWAO...YA MAZEMBE KUJIRUDIA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here