Home Habari za michezo BAADA YA USHINDI JANA NA KUINGIA NNE BORA EPL…ARTETA AANZA TAMBO …AJIKUTA...

BAADA YA USHINDI JANA NA KUINGIA NNE BORA EPL…ARTETA AANZA TAMBO …AJIKUTA NAYE NI ‘BAB KUBWA’..


Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ametamba baada ya kukiongoza kikosi chake kuondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Ham United na kutinga nne bora ya Ligi Kuu England mtanange uliopigwa jumapili katika dimba la London.

Kufuatia ushindi huo, Arteta amesema ni alama ya timu kubwa ya kushinda mechi hata kama timu haijacheza vizuri, tambo zinaendana na nafasi iliyopo klabu hiyo ya London.

The Gunners walijua wazi kuwa ushindi pekee ungewapa nafasi ya kwenda kushika nafasi ya nne kwani kabla yao Tottenham Hotspur walikuwa wameshinda bao 3-1 dhidi ya Leicester City.

Mabao ya Arsenal yamefungwa na walinzi, alianza Rob Holding akimalizia mpira wa kona wa Bukayo Saka dakika ya 38 kisha Wagonga Nyundo wa London West Ham wakasawazisha bao hilo kupitia kwa Jarrod Bowen

Dakika chache baada ya mapumziko, Arsenal walichukua uongozi tena kupitia bao la mlinzi mwenye miraba minne Gabriel Magalhaes, goli lililodumu mpaka dakika 90.

“Tumecheza vibaya lakini tumeshinda mchezo. Hivi ndivyo timu zote kubwa hufanya, hushinda hata bila ya kucheza vizuri”, alisema kocha Arteta ambaye karibuni alikuwa anahusishwa kujiunga na Paris St-Germain.

Kwa ushindi huo, Arsenal wanakuwa nyuma kwa alama tatu dhidi ya timu iliyonafasi ya tatu Chelsea ambayo jana mapema imekutana na kipigo cha bao 1-0 na kibonde Everton.

SOMA NA HII  MASTAA SIMBA WAFUNGIWA KUIWINDA VIPERS ....VIGOGO WAPANIA KUMALIZA KAZI MAPEMA....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here