Home Habari za michezo DEWJI AINGILIA KATI ISHU YA MOSES PHIRI NA ADEBAYOR KUTUA...

DEWJI AINGILIA KATI ISHU YA MOSES PHIRI NA ADEBAYOR KUTUA SIMBA…AAGIZA WASAJILIWE HARAKA….


Simba juzi ilikuwa mkoani Lindi ikipambana na Namungo ya huko katika mchezo wa Ligi Kuu Bara huku mjini kuna mfadhili wao mmoja mzito aliyewapa rekodi kubwa Afrika, Azim Dewji amevunja ukimya.

Akizungumza Azim alisema Simba haina uhakika wa kupata taji la ligi na tayari imeshatolewa hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika wakati huu ni muafaka mabosi wa klabu hiyo kuanza kufanya kazi kwa vitendo na sio maneno tena.

Azzim akifafanua zaidi alisema mabosi wa Simba kuanzia Mwenyekiti wa Bodi ya klabu hiyo, Salim Abdallah ‘Try Again’ na Rais wa heshima, Mohamed Dewji wanatakiwa kuanza kuisuka timu yao upya kulingana na mapungufu ya timu hiyo msimu huu.

Bosi huyo ambaye aliiongoza Simba kucheza Fainali ya Kombe la CAF Afrika alisema mabosi hao wanatakiwa kuanza kuwashusha mastaa wa kweli na sio kuishia kuwataja tu kina Victorien Adebayor na Mosses Phiri wa Zambia.

“Tumekuwa tukisikia majina tu mara Adebayor mara Phiri hizi taarifa sasa ziwe na mwisho kama hao wachezaji klabu imewaona ni wazuri kwa klabu yetu basi wasajiliwe haraka,” alisema Azim.

“Simba ya msimu huu tumeiona nafikiri sio siri tena kwamba kipi kinatakiwa kufanyika ili tupate timu bora kwa msimu ujao, hatukuwa na washambuliaji bora kama misimu michache iliyopita, kuna vijana wetu wamepungua ubora, lazima klabu ipate nguvu mpya.

“Huu sio wakati tena wa kusikia mambo ya siasa Simba imeshatoka huko, tuanze sasa kuishi kwa hesabu zinazokamilika na watu wakaona hapa kuna hatua kubwa inapigwa, tunatakiwa kurudi kwa nguvu msimu ujao.”

Azzim aliongeza kuwa kwa timu ambayo Simba ilikuwa nayo msimu huu ilikuwa hesabu ngumu kuona wanatinga hatua ya nusu fainali au fainali ambapo huko wanatakiwa kuwa na wachezaji bora wanaojua kuamua mechi ngumu dhidi ya timu ngumu.

“Msimu huu asilimia kubwa ya mabao yetu tumekuwa tukiyapata kwa viungo na sio washambuliaji, washambuliaji wetu walifunga lakini mabao machache sana, isingekuwa rahisi kutinga hatua ya nusu fainali au hata fainali ya CAF.

SOMA NA HII  YANGA :- SIMBA WAMEMKOSEA HESHIMA MANGUNGU....KWA NINI HAKUKAA NA RAIS SAMIA..?

“Tumeona jinsi timu ilivyocheza hapa dhidi ya Orlando Pirates ni vizuri tulishinda kwa bao moja lakini klwa ugumu ambao tulikutana nao ugenini na tulivyocheza kwa ubora kule, kama haoa tungeshinda kwa mabao ya kutosha tungefika kule tulikotaka kwahiyo hapa tumeshajifunza kwamba timu inataka nini, watu gani bora wa kuongeza,” alisema.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Kassim Dewji amesema kwamba watafanya usajili kwa utulivu kwa mujibu wa matakwa ya kocha na siyo papara.