Home Habari za michezo EHHEE…KUMBE LIGI KUU ENGLAND WALIKUWA HAWAJAMTAMBUA BOSI MPYA WA CHELSEA TU…WAMETOA WARAKA...

EHHEE…KUMBE LIGI KUU ENGLAND WALIKUWA HAWAJAMTAMBUA BOSI MPYA WA CHELSEA TU…WAMETOA WARAKA HUU….


Bodi ya Premier League imethibitisha mapendekezo ya kuuzwa kwa klabu ya Chelsea kwa Todd Boehly na washirika wake kama ilivyotangazwa jana jioni kwenye ligi hiyo.

Todd Boehly anayemiliki klabu ya Los Angeles Dodgers na washirika wake, wamekubali kulipa kiasi cha £4.25 bilioni kuinunua klabu hiyo kutoka kwa Roman Abramovich ambaye amekuwa akiimiliki kwa miaka 19 sasa.

Waraka wa Premier League uliotoka jana jioni unasomeka ” Bodi ya Premier League leo imethibitisha mapendekezo ya kuinunua klabu ya chelsea kwenda kwa Todd Boehly/Clearlake na washirika wake.

“Malipo yanabaki chini ya serikali ambao wanatoa kibali cha mauzo na kujiridhisha maridhiano ya mwisho hadi hatua ya malipo.”

SOMA NA HII  HAWA NDIO MASTAA HATARI DABI YA KARIAKOO