Home Habari za michezo MKUNDA AIKOSOA YANGA…. ADAI KUWA JAMBO HILI NI USHAMBA

MKUNDA AIKOSOA YANGA…. ADAI KUWA JAMBO HILI NI USHAMBA

Habari za Yanga leo

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Ahmad Mkunda amesema kuwa kitendo cha Klabu ya Yanga kuweka bango barabarani kuwazodoa wapinzani wao Simba Sc ni ushamba ambao umepitwa na wakati.

Mkunda amesema hayo baada ya Yanga kuweka bango barabarani linaloonyesha mabao 5-1 waliyowafunga wapinzani wao Simba, Novemba 5, 2023.

“Wanachokifanya Yanga kulipia gharama ya kuweka mabango barabani baada wakinadi ushindi wao wa 5-1 dhidi ya Simba huu ni ushamba. Ni bora waweke nguvu zaidi kujiandaa na Michezo Yao ya Hatua ya makundi ya Klabu Bingwa,” amesema Mkunda.

SOMA NA HII  PAMOJA NA YOTE...LAKINI HILI SIMBA HAMUMTENDEI HAKI MGUNDA....ACHENI HIZO BANA....