Home Habari za michezo ISHU YA KOCHA WA SIMBA YAFIKIA PATAMU

ISHU YA KOCHA WA SIMBA YAFIKIA PATAMU

Uongozi wa Simba SC umesema utamtangaza kocha wake mpya kabla haijacheza na ASEC Mimosas ya vory Coast katika mchezo wa kwanza wa Kundi B wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAFCL).

Simba SC itavaana na ASEC Mimosas Novemba 25 katika Uwanja Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Klabu hiyo ambayo juma lililopita ilitangaza kuachana na kocha wake mkuu, Roberto Oliveira na kocha wa viungo, Corneille Hategekimana, imeripotiwa kuwa tayari imeshapata Kocha mwingine.

Afisa Matendaji Mkuu wa Simba SC, Imani Kajula amesema mchakato wa kumpata kocha mpya umekamilika kwa asilimia 90 na hivi karibuni watamtangaza.

Kajula amesema mchakato huo haukuwa rahisi kwa kuwa walipaswa kumtafuta kocha bora anayejua vyema soka la Afrika na mwenye uwezo wa kutimiza malengo ya timu.

“Tupo katika mchakato wa mwisho kumalizana na kocha mpya na muda si mrefu tutamtambulisha, hivyo mashabiki na wapenzi wa timu yetu wala wasiwe nba wasiwasi kwani tutaleta kocha ambaye atakuwa na vigezo vya kuifundisha Simba SC, pia atatimiza malengo tuliyojiwekea,” amesema.

Hivi sasa, kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi kipo chini ya Kocha wa makipa, Daniel Cadena akisaidiwa na Selemani Matola ambaye awali alikuwa katika timu za vijana.

SOMA NA HII  HAWA HAPA WACHEZAJI MAJERUHI WA SIMBA NA YANGA WALIOPONA...LIST KAMILI HII HAPA