Home Habari za michezo BANGO LA YANGA LAIPELEKA SIMBA MAHAKAMANI

BANGO LA YANGA LAIPELEKA SIMBA MAHAKAMANI

Tetesi za Usajili Simba

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Simba na mjumbe wa kamati ya ushauri Ismail Aden Rage amesema kuwa viongozi wa timu hiyo wanapaswa kuwashitaki wapinzani wao, Yanga SC kwa kutumia logo yao katika bango waliloliweka jana likionesha matokeo waliowafunga Simba 5-1, Novemba 5, 2023.

Katika bango hilo, inonekana logo ya Simba na Yanga pamoja na logo za wadhamini wa Yanga ambao ni GSM, SportPesa, Hier, Azam, NIC pamoja na Saifi Store jambo ambalo linatafriwa kama ni biashara.

“Aliyeweka yale mabango ni kampuni ya Outdoor ambayo ni kampuni ya kibiashara, imeweka mabango na nembo ya Simba bila ruhusa yetu, nimewashauri viongozi kesho wachukue hatua za kisheria, tulipwe Th milioni (100) kwa kuchezea nembo yetu bila sababu ya maana.

“Hili tangazo limewekwa na kampuni ya Uutdoor, ni tangazo la kibiashara ambao wamekubaliana na Yanga, sisi hatuna tatizo na Yanga waweke matangazo vyovyote wanavyotaka lakini wasiweke tangazo la biashara.

“Kwa kuwa wameweka tangazo la biashara, sisi tunawadai watu wa Outdoor watulipe pesa sio Yanga,“ amesemsa Ismail Aden Rage.

Kwa upande wake, Wakili Lugomo kutoka ofisi ya mawakili ya Mzizima Advocates akiongea na Clouds FM amesema; “Hili suala la Yanga kuweka mabango kisheria sioni madai yoyote ambayo Simba anaweza kuwa nayo dhidi ya Yanga, Yanga wamechukua video ambayo imetengenezwa na Azam TV.

“Mwenye umiliki wa hayo maudhui ni Azam TV, TFF na Bodi ya ligi wameuza maudhui yote kwa Azam TV na wao wana exclusive right. Ukija kwenye uwanda huo Yanga wametumia maudhui ya Azam TV, mtu ambaye anaukalibu na hili ambaye angeweza kudai chochote ni Azam TV kama Yanga wameyatumia bila idhini yake,” amesema Lugomo.

SOMA NA HII  UNAKUMBUKA ZILE HABARI ZA SHONGA KUTUA SIMBA??... SASA MAMBO YAPO HIVI..!!!