Home Simba SC KUUMIA KWA DJUMA WA AS VITA SIMBA WATUMA SALAMU ZA POLE

KUUMIA KWA DJUMA WA AS VITA SIMBA WATUMA SALAMU ZA POLE

 


WAKATI wapinzani wa Klabu ya Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika,  AS Vita wakitarajiwa kutua leo Bongo kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao utakaochezwa Aprili 3, Uwanja wa Mkapa, Simba wametuma pole.


Salamu hizo za pole kwa Simba inayonolewa na Didier Gomes raia wa Ufaransa zinatokana na kuumia kwa beki wao wa kupanda na kushuka Djuma Shaban. 


Shaban aliwapa tabu Simba kwenye mchezo wa Kwanza wa hatua ya makundi uliochezwa nchini Congo na ubao kusoma AS Vita 0-1 Simba.


Ule upande anaocheza mzawa Mohamed Hussein ulipata tabu jambo ambalo lilimfanya Gomes awatumie viungo wake Luis Miquissone na Clatous Chama kuongeza nguvu ya kukaba.


Kupitia ukurasa wake rasmi wa Istagram Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema, “Pole sana Djuma Shaban, “.


Nyota huyo chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Florent Ibenge ataukosa mchezo wa pili utakaochezwa Uwanja wa Mkapa,  Aprili 3.

Katika mchezo huo Simba wenye pointi 10 katika kundi A wanakibarua cha kusaka pointi moja ili kutinga hatua ya makundi huku AS Vita wakiwa na uhitaji mkubwa wa pointi tatu mazima ili kufufua matumaini ya kutinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa kuwa akimalizana na Simba wana mchezo mwingine mkononi.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA SIMBA KUMBEBA FABRICE NGOMA JUU JUU AIRPORT...UKWELI WA JAMBO HUU HAPA...