Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA SIMBA KUMBEBA FABRICE NGOMA JUU JUU AIRPORT…UKWELI WA JAMBO...

KUHUSU ISHU YA SIMBA KUMBEBA FABRICE NGOMA JUU JUU AIRPORT…UKWELI WA JAMBO HUU HAPA…

Tetesi za Usajili Simba

Ni kweli kwamba uongozi wa Klabu ya Yanga walikuwa wanamhitaji Fabrice Ngoma raia wa Congo DR hapo awali tofauti na wapinzani wao, Simba Sc.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa, klabu hiyo ilianza mazungumzo na meneja wa mchezaji huyo Faustino Mukandila lakini hawakufikia muafaka licha ya mazungumzo kufikia pazuri na dili likawa halina muendelezo kwa Yanga.

Simba wakawasiliana na meneja wa Fabrice Ngoma Kisha wakafanya mazungumzo wakitaka kumsajili,meneja akawataarifu Yanga kuhusiana na Simba kumtaka Ngoma, Yanga wao wakampa ruhusa meneja ya kupokea ofa.

Taarifa zinaeleza kuwa kiongozi wa juu wa Yanga aliwasiliana na Kocha Florence Ibenge juu ya kumsajili Ngoma Kisha akapewa ushauri ambao ameutekeleza juu ya usajili huo.

Majeruhi yanatajwa kuwa ni kikwazo cha nyota huyo ambaye amewahi kuitumikia RS Berkanechini ya Ibenge.

Hii inafanana na dili Kama ambalo lilikuwa kwa Simba na Eric Kabwe ambao walifikia hatua nzuri kwenye mazungumzo ya kumsajili lakini baadae hawakuwa na muendelezo mzuri Kisha akasajiliwa Uarabuni..

Hivyo Yanga hawajapokonywa mchezaji Airport ila ni mambo tu ya Simba na Yanga kama kawaida yao, ukipata nafasi mtambie mwenzako.

SOMA NA HII  ROBERTINHO AFUNGUKA HALI YA WACHEZAJI WA SIMBA HUKO UTURUKI SIO POA.......ISHU IKO HIVI

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here