Home Habari za michezo MASTAA SIMBA WAFUNGUKA KUHUSU UGAMVI UNAOENDELEA KWENYE KLABU HIYO

MASTAA SIMBA WAFUNGUKA KUHUSU UGAMVI UNAOENDELEA KWENYE KLABU HIYO

Habari za Simba

Nyota wa Zambia anayechezea Simba SC, Clatous Chama amesema anakiri kwamba hawakucheza vizuri kwenye michezo mitatu iliyopita lakini si kwamba kuna ugomvi ndani ya timu.

Chama amesema, kwa sasa Simba hawatakiwi kunyosheana vidole na badala yake waungane, waisapoti timu ili waweze kurudi kwenye matokeo yao ya kuwapa furaha Wana-Simba.

“Msimu uliopita Champion League tulianza vibaya, tulipoteza dhidi ya Horoya, tukaja tukapoteza dhidi ya Raja lakini baadaye tuliamka na kupata matokeo yaliyotuwezesha kuvuka kwenda hatua iliyofata ya Robo Fainali,” alisema Chama.

Simba wamekuwa na wakati mbaya baada ya kupoteza michezo mitatu iliyopita kwa mmoja kufungwa na Yanga, miwili sare dhidi ya Namungo FC (1-1) na dhidi ya ASCE Mimosas (1-1).

SOMA NA HII  SIMBA KAZI BADO IPO LEO TAIFA MBELE YA SINGIDA UNITED