Home Habari za michezo KISA UBAHILI…KIUNGO MKATA UMEME AIKIMBIA SIMBA…AFUNGUKA A-Z WALIVYOKUBALINA…

KISA UBAHILI…KIUNGO MKATA UMEME AIKIMBIA SIMBA…AFUNGUKA A-Z WALIVYOKUBALINA…

Habari za Simba SC

Simba ni kama imenyang’anywa tonge mdomoni na Singida Big Stars baada ya Walima Alizeti hao kukamilisha usajili wa kiungo fundi, Kelvin Nashon kutoka Geita Gold aliyekuwa anakaribia kutua Msimbazi, huku mwenyewe akisema Simba walichelewa wenyewe.

Simba ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kumfuata Nashon kwa mazungumzo ikitaka kumsajili na kukubaliana kila kitu ikiwemo pesa ya usajili na mshahara, muda wa mkataba na marupurupu mengine lakini ghafla kiungo huyo ametua Singida Big Stars na sababu kubwa ikielezwa kuwa ni maslahi.

Mmoja kati ya watu wa karibu na Nashon aliyehusika kwenye kukamilisha dili hilo la kutua Singida amesema kuwa, Nashon na Simba walimalizana kila kitu ikabaki kuingiziwa pesa kwenye akaunti yake tu ili amwage wino wa kuwatumikia Wana Msimbazi hao lakini vigogo hao wa Kariakoo wakachelewesha malipo hayo ndipo Singida ikamchukua kiulaini.

Nashon tayari alikuwa ameshaaga Geita na kuwaambia baadhi ya wachezaji wenzake anaenda Simba lakini Singida ikagundua kinachosubiriwa ni pesa kuingia kwenye akaunti ndio ikatumia nafasi hiyo na kummwagia mkwanja mrefu kisha akasaini.

“Nashon mwanzoni alijua anakwenda Simba, lakini walichelewa kumuingizia pesa na muda huohuo akiwa hajatulia ndipo Singida ikaja na pesa keshi na kumchukua,” kilieleza chanzo chetu na kuongeza;

“Siyo kwamba pesa ya Singida ni kubwa kuliko ile ya Simba, lakini mchezaji mwenyewe amecheza na muda kwani ukute wangemwambia wanamwekea pesa na wasiweke hadi dirisha la usajili linafungwa na akawa amekosa vyote.”

Aidha inasemekana kuwa Nashon ameogopa kuchezea fursa kama ilivyokuwa misimu miwili nyuma akiwa JKT Tanzania ambapo alipata ofa kibao ikiwamo ya Azam FC na Namungo za mkwanja mrefu lakini aligoma kujiunga nao kwani JKT ilikuwa imemuahidi ajira ya Jeshi na baadaye akakosa vyote.

Nashon ambaye anatajwa kati ya viungo bora hapa nchini amekiri kuongea kila kitu na Simba lakini ameamua kujiunga na Singida kwakuwa ndiyo iliyokuwa makini zaidi.

“Simba niliongea nao na tukafika sehemu nzuri lakini wakawa kama wanasita kuweka pesa, Singida wamekuja mara moja na tukamaliza kila kitu,” alisema fundi huyo wa Taifa Stars na kuongeza;

“Nafurahia hapa, naamini ni sehemu salama kwangu na kwa kiwango changu na kwa kushirikiana na wenzangu nimejipanga kuisaidia timu kufikia malengo.”

Simba kwa sasa ipo Dubai kwa kambi maalumu ya siku 10 lakini ikiwa huko imeendelea kutafuta kiungo wa kati mwenye uwezo mkubwa wa kukaba na kuchezesha timu baada ya kumkosa Nashon na yupo na timu hiyo visiwani Zanzibar akisubiri kucheza fainali ya Kombe la Mapinduzi.

Mpaka sasa Simba imemsajili mchezaji mmoja tu kwenye dirisha hili, Saido Ntibazonkiza.

SOMA NA HII  KOCHA MPYA YANGA HUYU HAPA....HIYO CV YAKE TU..MBRAZILI WA SIMBA AKASOME UPYA...