Home Simba SC KONDE BOY WA SIMBA CHAGUO LA GOMES ATAJA KINACHOMPA FURAHA

KONDE BOY WA SIMBA CHAGUO LA GOMES ATAJA KINACHOMPA FURAHA


 LUIS Miquissone,  kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Simba amesema kuwa anachofurahia ndani ya uwanja ni juhudi na kuona timu inapata matokeo chanya. 


Miquissone ni chaguo la kwanza kwa Kocha Mkuu, Didier Gomes ana tuzo moja ya mchezaji chaguo la mashabiki kwa mwezi Februari pia katika Ligi ya Mabingwa Afrika bao lake alilowatungua Al Ahly lilichaguliwa kuwa bao bora.


Bao hilo alifunga akiwa nje ya 18 kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Al Ahly akimalizia pasi ya mshikaji wake Clatous Chama. 

Kwa sasa kikosi cha Simba kinajiandaa kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya AS Vita unaotarajiwa kuchezwa Aprili 3, Uwanja wa Mkapa.

Walipowafuata DR Congo,  ubao ulisoma AS Vita 0-1 Simba na mpachika bao alikuwa ni Chris Mugalu kwa penalti iliyosababishwa na Luis wengi wanapenda kumuita Konde Boy. 

Nyota huyo amesema:”Ninapenda kuona timu inapata matokeo, ninapenda kufanya juhudi muda wote na kila wakati, mashabiki wazidi kutupa sapoti,” . 

SOMA NA HII  KWA TAARIFA YAKO..ILE ISHU YA CHAMA KURUDI TZ...IKO SAWA SAWIA NA ISHU ZA OKWI KURUDI SIMBA...