Home Habari za michezo FEI TOTO AFUNGUKA YAKE NA YANGA….ADAI IWE ISIWE LAZIMA KIELEWEKE…AGUSIA ALIVYOVUMILIA…

FEI TOTO AFUNGUKA YAKE NA YANGA….ADAI IWE ISIWE LAZIMA KIELEWEKE…AGUSIA ALIVYOVUMILIA…


Kiungo kutoka visiwani Zanzibar na klabu ya Young Africans Feisal Salum ‘Fei Toto’ amesema msimu huu ana uhakika wa kumaliza kiu yake ya kutwaa taji la Ligi kuu, baada ya kushindwa kufanya hivyo tangu aliposajiliwa akitokea JKU.

Faisal ni miongoni mwa wachezaji waliocheza kwa muda mrefu katika kikosi cha sasa cha klabu hiyo, lakini alikua na ukame wa furaha ya ubingwa, tangu alipoanza kucheza katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara, huku akishuhudia majirani zao Simba SC wakifurahia kwa misimu miNne mfululizo.

Kiungo huyo amesema kutokana na juhudi na mipango iliopo klabuni kwao kwa sasa, hana shaka sana na suala la ubingwa kama ilivyokua mIsimu iliyopita, hivyo anasubiri muda ili afurahie ubingwa wake wa kwanza akiwa Young Africans

“Kweli sijabeba ubingwa tangu nijiunge na Young Africans lakini msimu huu iwe isiwe lazima nibebe ubingwa.”

“Nafahamu ni suala la muda tu, ili kufikia lengo la kutwaa ubingwa nikiwa na klabu hii kwa mara ya kwanza, uvumilivu wangu kwa mara ya kwanza unaanza kunionyesha nuru ya furaha ya ubingwa.”

“Na hii sio kwangu tu, najua hata kwa mashabiki wa Young Africans nao watakua na hamu kubwa ya kurudisha furaha iliyopotea kwa muda mrefu, na ndio maana wamekua mstari wa mbele kutupa ushirikiano kila tunapokua Uwanjani tukipambana.” Amesema Feisal Salum.

Young Africans iliyocheza michezo 22 ya Ligi Kuu hadi sasa, inaongoza msimamo wa Ligi hiyo ikiwa na alama 56, ikiiacha kwa tofauti ya alama 13 Simba SC inayoshika nafasi ya pili.

SOMA NA HII  SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU KUZUIWA KWA NAMUNGO NA JESHI ANGOLA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here