Home Habari za michezo ILE ISHU YA PABLO KUTAKIWA NA ORLANDO…WAKALA WAKE MKENYA AIBUKA NA KUANIKA...

ILE ISHU YA PABLO KUTAKIWA NA ORLANDO…WAKALA WAKE MKENYA AIBUKA NA KUANIKA KILA KITU WAZI…


Wakala wa Kocha Mkuu wa Simba, Pablo,  Mkenya Edgar Mitema amesema hatima ya mteja wake iko mikononi mwa viongozi wa klabu hiyo.

Akizungumza kutoka nchini Kenya, Mitema alisema kocha huyo anatakiwa na klabu nyingi kwa sasa, na si Orlando Pirates ya Afrika Kusini pekee bali hata Horoya ya Guinea ni miongoni mwa zinazohitaji huduma yake, lakini bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Klabu ya Simba, hivyo ili klabu zinazomhitaji zimpate, ni lazima maamuzi yatoke kwa viongozi hao.

Wakati Mitema akisema hayo, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Murtaza Mangungu amesema kwa sasa hawawezi kusema lolote mpaka hapo ligi itakapomalizika, pamoja na Kombe la FA na baada ya hapo watakaa chini na kuangalia mafanikio yaliyopatikana kwanza.

“Kulikuwa na ofa ya Orlando Pirates kabla hata ya droo ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho, kulikuwa na ofa nyingine Horoya, lakini ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba, hivyo ni lazima tuheshimu mkataba. Ofa ziko nyingi, lakini tutaangalia mwishoni kama Simba inataka kumbakisha au la, hilo tutajadiliana mwishoni mwa msimu,” alisema wakala huyo raia wa Kenya.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, Mangungu alisema kutokana na uwezo aliouonyesha raia huyo wa Hispania, haishangazi kuona klabu nyingi zikivutiwa naye, lakini akaongeza kuwa mkataba ni hiari kati ya mwajiri na mwajiriwa, na huwa na vipengele vyake kwa faida kwa pande zote mbili.

SOMA NA HII  SIMBA MBONA INAFUZU KIBOSI TU.... AKILI YA ROBERTINHO IKO HIVI