Home Habari za michezo KAZE : TULITUMIA NGUVU KUBWA SANA KWENYE MECHI DHIDI YA SIMBA…

KAZE : TULITUMIA NGUVU KUBWA SANA KWENYE MECHI DHIDI YA SIMBA…


Vinara wa ligi kuu Tanzania bara (Nbc Premier League 2021/22) klabu ya Yanga wanatarajiwa kushuka kwenye dimba la Lake Tanganyika mnamo May 4 kupambana na klabu ya Ruvu Shouting majira ya saa kumi kamili jioni.

Kocha msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema hakuna ongezeko la wachezaji walio majeruhi tofauti na wachezaji wawili (Chiko Ushindi na Yacouba Sogne) huku wakitambua kila wakicheza na Ruvu Shouting mchezo huwa mgumu.

“tunaingia kwa tahadhari kubwa,tumetumia nguvu kubwa kwenye mechi dhidi ya Simba ,tunajua umuhimu wa mechi ya kesho kama ni mechi ngumu na tunafahamu pindi tukicheza na Ruvu Shooting mechi huwa ngumu kwa hiyo tunaingia kwa tahadhari kubwa “amesema Kaze

Mpaka sasa Yanga imejikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Tanzania bara wakiwa na alama 55 kwenye michezo 21 waliyocheza huku Ruvu Shouting wakikamata nafasi ya 14 wakiwa na alama 21 kwenye michezo 20 waliyocheza mpaka sasa huku mara ya mwisho Yanga kucheza kwenye uwanja huo ilikuwa ni kwenye mchezo wa kombe la FA msimu wa 2020/21

SOMA NA HII  KOCHA WA CHELSEA KUWAPA MAUJANJA CHAMA NA PHIRI....ISHU IKO HIVI..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here