Home Habari za michezo KISA KUPEWA POINTI ZA ‘MEZANI’…JULIA ‘ABUBUJIKWA’ NA HAYA BAADA YA KUPATA...

KISA KUPEWA POINTI ZA ‘MEZANI’…JULIA ‘ABUBUJIKWA’ NA HAYA BAADA YA KUPATA POINTI 6 SIKU MOJA…


KOCHA Msaidizi wa Namungo FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ameonyesha kufurahishwa na timu yake kupata pointi sita kwa siku moja, wakati ikiichapa Biashara United mabao 2-1 juzi kwenye Uwanja wa Nyamagana Mwanza  uamuzi wa kupewa pointi tatu na mabao matatu na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), ukitolewa kutokana na Mbeya Kwanza kugomea mechi.

Akizungumza baada ya mechi hiyo kumalizika, alisema yeye, wachezaji wake na viongozi wamefurahi kupata pointi tatu ugenini dhidi ya Biashara United kwa sababu wamezitolea jasho uwanjani, huku wakitoka safari ya mbali mkoani Lindi hadi Mwanza kwa ajili ya kuzisaka.

“Tunashukuru Mungu, tumetoka safari ya mbali sana, kutoka Lindi hadi Mwanza, tukapata pointi tatu ni jambo la kushukuru na kujisikia faraja,” alisema.

Yalikuwa ni mabao ya Shiza Kichuya dakika ya nane na 67, yakiiwezesha timu hiyo kupata ushindi huo, huku la kufutia machozi la Biashara United inayotumia uwanja huo, likifungwa na Ambrose Awio.

Wakati wakipata pointi hizo tatu, Namungo ikaongezewa pointi zingine kama hizo juzi baada ya Kamati ya TPLB kuipa ushindi kutokana na Mbeya Kwanza kugomea mchezo kwa madai ya kutokuwapo kwa gari la wagonjwa uwanjani na hata lilipokuja, muda wa kikanuni ulikuwa umepita.

Kamati ilidai baada ya kupokea taarifa, ilifanya uchunguzi na kubaini gari hilo lenye namba STL 3096 lilifika uwanjani hapo, lakini liliondoka kwa dharura kabla ya muda wa mchezo.

Ikasema waandaaji wa mchezo, Chama cha Soka Lindi kwa kushirikiana na kamisaa wa mchezo walikubaliana kutafuta gari linaloweza kutumika kubeba majeruhi kabla gari hilo maalum halijarejea, lakini Mbeya Kwanza walipinga, pamoja na gari hilo kurejea kabla ya muda.

Julio alisema walistahili kupata pointi hizo, na pia alitegemea kwa sababu wenzao hawakutaka kucheza mpira, ila kutafuta pointi za mezani.

“Wachezaji wao walitaka kucheza, lakini baadhi ya viongozi hao wakapinga kabisa, wakagomea, tuliathirika kwa sababu tuliingia gharama ya kujiandaa na mchezo huo, hivyo tumestahili,” alisema.

SOMA NA HII  WAKATI AKIWA KWENYE LISTI YA WANAOACHWA ...NTIBAZONKIZA APATA WATETEZI...YANGA YAPEWA ONYO...

Kwa matokeo hayo, Namungo imefikisha pointi 36, ikiwa kwenye nafasi ya tatu ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here