Home Habari za michezo KISA SARE MICHEZO MIWILI ILIYOPITA…NABI AFURA KWA ASIRA YANGA…ATOA MKWARA HUU KWA...

KISA SARE MICHEZO MIWILI ILIYOPITA…NABI AFURA KWA ASIRA YANGA…ATOA MKWARA HUU KWA WACHEZAJI…


Kocha Mkuu wa Young Africans Nesreddine Nabi amezidisha ukali kwa wachezaji wake ambapo amewataka kupambana na kufikiria kama wanaanza msimu ili kupata matokeo mazuri katika michezo yao minane iliyobakia ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Michezo iliyobaki ni dhidi ya Tanzania Prisons, Dodoma Jiji, Mbeya Kwanza, Biashara United, Coastal Union, Polisi Tanzania, Mbeya City na Mtibwa Sugar.

Nabi amesema ameamua kubadili fikra zao baada ya kuona wachezaji wake wanaonekana kuridhika au wakiamini wameshamaliza kazi kutokana na namna walivyocheza katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Simba na Ruvu Shooting.

Nabi amesema bado hawajafikia malengo ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na baada ya kutoka suluhu na Simba wachezaji wakawa wameridhika jambo ambalo halijamfurahisha.

“Wachezaji wanatakiwa kujitoa na kupambana zaidi ya hapo, lengo ni kutwaa ubingwa wa ligi, sitaki kuona mchezaji yoyote anacheza kwa kuridhika na kuondoa ule ubora wake aliokuwa nao kabla ya mchezo dhidi ya Simba,” amesema Nabi.

Amesema anahitaji wachezaji kujitoa zaidi katika michezo iliyobaki ili kuzipata pointi hizo wanazozihitaji ambazo hazitafikiwa na timu yoyote katika mbio hizo za kuwavua ubingwa wapinzani wao, Simba.

Kocha huyo amesema wanahitaji kuweka rekodi nyingine ikiwamo kuchukua ubingwa kwa idadi kubwa ya pointi na mabao mengi ya kufunga pia ikiwezekana wamalize msimu bila ya kupoteza mechi hata moja.

“Baada ya kurejea jijini, tumerudi uwanjani kwa ajili ya kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika michezo miwili iliyopita na kujiweka sawa na mechi iliyopo mbele yetu dhidi ya Tanzania Prisons,” alisema kocha huyo.

Young Africans itashuka tena dimbani leo Jumatatu (Mei 09) kuwakaribisha Tanzania Prisons kuanzia saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

SOMA NA HII  JONAS MKUDE AANZA RASMI KUFANYA MAAJABU YAKE KATIKA KIKOSI CHA YANGA, MCHEKI AKIWA KAMBINI