Home Habari za michezo KISA SARE NA YANGA JANA…PABLO ‘KAFURA KWA HASIRA’ SIMBA…ADAI WALIKUWA WANAUHAKIKA WA...

KISA SARE NA YANGA JANA…PABLO ‘KAFURA KWA HASIRA’ SIMBA…ADAI WALIKUWA WANAUHAKIKA WA USHINDI…


Kocha Mkuu Pablo Franco, amesema hajafurahishwa na sare ya bila kufungana  dhidi ya Yanga kwa kuwa lengo  lilikuwa tupate pointi zote tatu.

Pablo amesema alama tatu zingetufanya kuwasogolea zaidi lakini matokeo hayo yamewafanya wapinzani wao kuwa karibu na ubingwa ingawa hatutakata tamaa mpaka mwisho.

Akiuzungumzia mchezo wenyewe Pablo amesema ulikuwa mzuri uliotawaliwa na mbinu ingawa walipaswa kutumia vizuri nafasi walizopata.

Pablo ameongeza kuwa hakuna muda wa kupumzika kwa kuwa maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya Namungo siku tatu zijazo yanapaswa kuanza mara moja.

“Sijafurahishwa na matokeo ya sare, tuliingia uwanjani kwa dhamira ya kutafuta ushindi kwakuwa tunahitaji kupunguza tofauti iliyopo na bado tunahitaji kutetea ubingwa wetu.

“Tunacheza mchezo ujao ugenini dhidi ya Namungo siku tatu zijazo kwa hiyo tunajiandaa na safari ingawa hatuna muda wa kutosha wa maandalizi ya mechi,” amesema Pablo.

SOMA NA HII  MBWANA SAMATTA ACHEKA NA NYAVU TIMU YAKE IKIFUNGWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here