Home Habari za michezo KISA TABIA ZAKE ZA ‘KIHUNI’ NDANI NA NNJE YA UWANJA…SIMBA YATAKIWA KUMPA...

KISA TABIA ZAKE ZA ‘KIHUNI’ NDANI NA NNJE YA UWANJA…SIMBA YATAKIWA KUMPA ADHABU HII MORRISON…


Mtangazaji wa kipindi cha Dimbani kutoka TV3, Alex Ngereza amesema kuwa kwa mwenendo wa tabia ya mchezaji wa Simba Sc, Bernard Morrison anapaswa kuadhibiwa vikali kutokana na vitendo vyake vya utovu wa nidhamu ndani na nje ya Uwanja.

Ngereza amesema Morrison amekuwa na mwendelezo wa matukio ya kihuni kama si jambo ambalo halipaswi kufanywa na mchezaji professional kama yeye.

“Morrison anashusha brand ya Simba, hakupaswa kupigana na shabiki, vitu anavyovifanya ni lazima Simba wampe adhabu Morrison” amesema Alex Ngereza.

Morrison alishikiliwa na jeshi la polisi katika Kituo cha Chang’ombe Temeke, kwa tuhuma za kumshambulia shabiki wa Yanga baada ya mchezo wa Derby ya Kariakoo (Yanga vs Simba) uliopigwa Jumamosi, Aprili 30, 2022 na kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

SOMA NA HII  WAKATI MATANGAZO YAKIWA 'LIVE'... BBC WAIITA MAN UTD TAKATAKA...CEO WAO AFICHUA ALIYEFANYA MCHEZO HUO...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here