Home Azam FC KUELEKEA MECHI YAO NA COASTL UNION LEO…KOCHA MSOMALI WA AZAM APANGA KUINGIA...

KUELEKEA MECHI YAO NA COASTL UNION LEO…KOCHA MSOMALI WA AZAM APANGA KUINGIA NA GIA ZA SIMBA….


Kocha mkuu wa timu ya Azam FC,Abdi Hamid Moallin amefunguka kuwa kwa  namna ambavyo amekiandaa kikosi chake anaamini mchezo wa leo Jumapili Mei 29 dhidi ya Coastal Union watashinda na kujitengenezea mazingira mazuri ya kwenda kimataifa.

Mchezo huo wa nusu fainali ya kombe la shirikisho la Azam Sports kati ya Coastal Union FC dhidi ya Azam FC itapigwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid hapa jijini Arusha ambapo mpaka sasa maandalizi yake yamekamilika.

Moallin amesema mchezo wa leo utakuwa na burudani ya aina yake kutokana na ubora wa wapinzani wao na anaamini hautakuwa mwepesi kwao lakini kwa namna ambavyo amekiandaa kikosi chake ushindi ni uhakika.

Amesema anawaheshimu wapinzani wao na hakuna ambaye ameingia nusu fainali kwa viti maalum kila mmoja amepambana kwa njia zake ukizingatia hii ni hatua ya mtoano lakini ili kufikia malengo lazima wamfunge Coastal na kwenda fainali.

“Tutawatumia Coastal kama daraja kwetu lazima tumfunge ndio tujitengenezee mazingira mazuri ya kwenda kimataifa”amesema Moallin.

Ameongeza kuwa kipaumbele kwake ni mchezo wa nusu fainali kwani katika ligi tayari ubingwa wameikosa kama mwalimu amekiadaa kikosi kushinda na kwenda huko ambako itakuwa rahisi kwao kuiwakilisha nchi kimataifa msimu ujao.

SOMA NA HII  AZAM FC WAMPA DILI LA MWAKA MMOJA BEKI MCAMEROON