Home Habari za michezo KUHUSU MBIO ZA UBINGWA MSIMU HUU…PABLO AISHTAKIA YANGA KWA MUNGU…AWAOMBEA MABAYA…

KUHUSU MBIO ZA UBINGWA MSIMU HUU…PABLO AISHTAKIA YANGA KWA MUNGU…AWAOMBEA MABAYA…


KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, raia wa Hispania, amefichua kuwa kilichobaki kwa sasa ni kuendelea kuwaombea wapinzani wao Yanga waendelee kupata matokeo mabaya huku wao wakiendelea kufanya vizuri kwa malengo ya kutwaa ubingwa wa msimu huu.

Pablo ametoa kauli hiyo kufuatia Simba kufikisha pointi 49 ikiwa ni tofauti ya pointi nane na vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga, wanaoongoza kwa pointi 57 baada ya suluhu tatu mfululizo.

Pablo alisema wanachokifanya kwa sasa ni kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi katika kila mchezo huku wakiendelea kuwaombea mabaya wapinzani wao katika michezo iliyobakia kabla ya kumaliza ligi.

Pablo Franco Martin amesema anaiombea mabaya klabu ya Yanga iendelee kudondosha alama kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara

“Tumebakisha pointi nane ili kuweza kuwafikia, bado ni pointi nyingi kulingana na mechi ambazo zimabakia kabla ya kumaliza ligi, japo kwa sasa tukiwa sawa kwa idadi ya mechi ambazo tumecheza lakini kitu kikubwa tunachokiangalia ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo ambao upo mbele yetu.

“Hatuwezi kukata tamaa ya ubingwa ikiwa wapinzani wameanza kupata matokeo mabaya kitu ambacho tunaomba kiendelee ili kupunguza pengo la pointi ambalo bado tupo nalo na kuweza kufikia malengo ya kutwaa ubingwa kwa sababu bado upo wazi, kila mmoja anaweza kutwaa, ndiyo maana tunaendelea kupambana,” alisema Pablo.

SOMA NA HII  TAMU NA CHUNGU WANAZOPITIA MASTAA WAPYA WA AZAM HIZI HAPA....SIMBA MTAPIGIKA....