Home Uncategorized HATMA YA AZAM FC KUTINGA ROBO FAINALI KAGAME MIKONONI MWA MUKURA FC

HATMA YA AZAM FC KUTINGA ROBO FAINALI KAGAME MIKONONI MWA MUKURA FC

ETTIENE Ndayiragije, Kocha wa Azam FC amesema kuwa suluhu waliyoipata leo kweye michuano ya Kagame dhidi ya Bandari inawaweka kwenye wakati wa kusubiri hatma yao ya kutinga hatua ya robo fainali.

Leo Azam FC walikuwa wanahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi ya kutinga robo fainali wameambulia suluhu ya kutofungana dhidi ya Bandari.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ndayiragije amesema kuwa ushindani ni mkubwa na kila timu ilikuwa inahitaji matokeo hivyo watasubiri mchezo wa mwisho kujua hatma yao.

“Hatujafanya vibaya, bado tuna matumaini ya kupenya robo fainali kwa kutegemea matokeo ya mchezo wa mwisho kati ya Mukura dhidi ya KCCA.

“Hivyo endapo Mukura watapoteza basi tutakuwa tumejihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali,” amesema.

Kwenye kundi B, ambalo Azam ipo, timu ya KCCA inashika nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 4 huku Azam FC nao wakiwa nafasi ya pili na wana pointi nne baada ya kucheza michezo mitatu, Mukura ana pointi moja na amecheza michezo miwili.

SOMA NA HII  MNAMIBIA WA YANGA AKWAMA KWAO