Home Uncategorized DIDA NAYE MGUU NJE NDANI SIMBA, ATAJWA KUIBUKIA NAMUNGO

DIDA NAYE MGUU NJE NDANI SIMBA, ATAJWA KUIBUKIA NAMUNGO

IMEELEZWA kuwa mlinda mlango namba mbili wa Simba, Deogratius Munish ‘Dida’ anaweza kusepa ndani ya kikosi hicho na kutimkia Namungo FC.

Habari zimeeleza kuwa kwa sasa, Dida anamalizia mkataba wake wa mwaka mmoja ndani ya Simba hivyo kusajiliwa kwa Beno Kakolanya kunampoteza ndani ya kikosi hicho.

Kakolanya amesaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya Simba akiwa ni mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba wake na mabosi wa Yanga.


Kocha wa Namungo FC, Hitimana Thiery amesema kuwa mpango mkubwa ni kupata wachezaji wenye uzoefu watakaoleta ushindani.

“Ushindani ni mkubwa na mpango wa timu ni kuleta wachezaji wenye uzoefu, kuhusu Dida mambo bado kwa sasa,” amesema.

SOMA NA HII  KIUNGO WA YANGA HUMWAMBII KITU KUHUSU UGALI