BEKI wa Yanga, Haji Mwinyi, huenda akatua Polisi T
anzania iliyo chini ya Suleman Matola ambaye amesaini kandarasi ya mwaka mmoja.
Mwinyi kwa sasa yupo huru kusaini na timu yoyote baada ya mkataba wake kumalizika ndani ya Yanga.
Pia imeelezwa kuwa Polisi Tanzania ya Matola ina mpango wa kumsajili beki wa Lipuli, Haruna Shamte ambaye ni fundi wa kupiga mipira iliyokufa ambapo ana mabao matatu aliyofunga kwenye michuano ya kombe la Shirikisho.