Home Uncategorized MNAMIBIA WA YANGA AKWAMA KWAO

MNAMIBIA WA YANGA AKWAMA KWAO


Wakati kikosi cha Yanga kikiwa kimeingia kambi rasmi juzi Jumatatu, nyota wa kigeni wa klabu hiyo, raia wa Namibia, Sadney Khoetage Urikhob ameshindwa kuripoti kwa wakati kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia.

Yanga ilianza kambi yake siku ya Jumatatu mjini Morogoro ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa ligi ambao unatarajiwa kuanza Agosti 23, mwaka huu.

Wachezaji wameingia rasmi kambini na wachezaji wale wapya wa kigeni ambao wapo kambini, Farouk Shikhalo (ambaye naye hajaripoti), Issa Bigirimana, Patrick Sibomana, Lamine Moro, Mustapha Suleiman, Juma Balinya, Maybin Kalengo huku wale wa ndani wapya ni pamoja na Ally Ally, Abdulaziz Makame, Muharami Issa na Balama Mapinduzi.

Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten alisema kuwa wachezaji tayari wameenda kambini tangu Jumatatu kwa ajili ya kuanza maandalizi.

Ten alisema wachezaji wa kigeni ambaye hajaripoti na ataripoti wakati wowote ni Sadney ambaye ana matatizo ya kifamilia, ndiyo maana amechelewa. “Wachezaji wote wapo kambini na wale wapya ambao wamesajiliwa, amekosekana mmoja ambaye ni Sadney aliyepo kwao Namibia kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia na atarejea hivi karibuni.

“Wale wachezaji ambao wote mwalimu aliwahitaji kwenye kikosi, wamepatikana baada ya kusajiliwa kwa ajili ya msimu ujao, hivyo matumaini yetu kuelekea msimu mpya ni kufanya vizuri.

“Na wachezaji wale ambao walikuwa kwenye timu za taifa, wao wamepewa muda wa kupumzika mpaka pale Julai 14, mwaka huu ndipo watakuwa na wenzao kuendelea na maandalizi huku kocha (Zahera) naye akitarajiwa kuingia wakati wowote nchini,” alisema Ten.

SOMA NA HII  LIONEL MESSI ANABALAA KWENYE SUALA LA POCHI NENE, CR 7 HAONI NDANI