Home Habari za michezo MANARA AMKARIBISHA RASMI MORRISON YANGA…’KAMCHANA LIVE’ KUHUSU TABIA ZAKE MBAYA…

MANARA AMKARIBISHA RASMI MORRISON YANGA…’KAMCHANA LIVE’ KUHUSU TABIA ZAKE MBAYA…


Msemaji wa Klabu ya Yanga, Hamis Manara ameandika haya baada ya mchezaji Bernard Morrison raia wa Ghana kuondoka ndani ya kikosi cha Simba.

“Kila la kheri huko uendako. kwa taarifa nilizopata mida hii, najulishwa unaelekea Club kubwa Barani Afrika, Sijajua ni Team gani,,ila najua ni Club ya kisawasawa ndani ya Continental hili kubwa.

“Lecturer Bernard Morrison Insha’Allah utapata University ya kweli soon. Ila chonde chonde huko uendako, tabia tumia za Hersi Said, Busara tumia za Senzo Mbatha na Maarifa tumia ya Bugati, zako mwenyewe ziache ulipotoka Morrison.”

Jana klabu ya Simba ilitangaza kumpa mapumziko ya hadi mwisho wa msimu huu, Morrison ambapo pia walimtakia kila la kheri kwenye maisha yake ya soka.

Wadadisi wa mambo wanadai kuwa Yanga SC ni klabu pekee iliyoonyesha na ambayo pia ipo kwenye nafasi kubwa ya kumsajili.

Pengine ujumbe huo wa Manara ni ishara tosha ya kuwa Morrison yupo njiani kurudi Yanga, ambayo nayo ni moja ya klabu kubwa Afrika.

SOMA NA HII  HII HAPA 'MOVE' YA YACOUBA NA YANGA....GEITA GOLD 'WATENGA NDOO BAHARINI' .....MWENYEWE AJIFIKIRIA NA 'SITAKI NATAKA'...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here