Home Habari za michezo MAN CITY WAMFANYIA KUFRUA YA DUNIA HAALAND…KUMLIPA MSHAHARA WA BILIONI 5 KWA...

MAN CITY WAMFANYIA KUFRUA YA DUNIA HAALAND…KUMLIPA MSHAHARA WA BILIONI 5 KWA WIKI…


MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Borussia Dortmund raia wa Norway Erling Braut Haaland amefuzu vipimo vya afya tayari kujiunga na klabu Ligi Kuu ya Uingereza Manchester City.

Haaland amefanyiwa vipimo hivyo nchini Ubelgiji na kwa mujibu wa taarifa ni kwamba mshambuliaji huyo tayari amesharejea kwenye kikosi cha Dortmund.

Taarifa zinasema Manchester City waliitaarifu Dortmund kuwa wapo tayari kutoa kiasi cha Euro Milioni 60 na siyo 75 ambazo ndiyo zinatakiwa kwa ajili ya kuvunja mkataba wake.

Mkataba wa mshambuliaji huyo unamruhusu kuondoka klabuni hapo kwa kiasi cha Euro Milioni 75 la sivyo ataondoka bure mwisho wa msimu ujao.

Haaland anatarajiwa kupokea zaidi ya Bilioni moja kwa wiki pesa ya Kitanzania kama sehemu ya mshahara wake akiwa na klabu ya Manchester City

Haaland anatarajiwa kupokea mshahara wa Paundi 375,000 kwa wiki ambayo ni sawa na Bilioni moja na milioni Sabini na Nne Laki Nane Arobaini na Mbili Elfu na Mia Mbili Sitini na Nane (1074842268) pesa taslimu ya Kitanzania ambayo ni karibu na bilioni 5 kwa mwezi.

SOMA NA HII  KAZE : TULITUMIA NGUVU KUBWA SANA KWENYE MECHI DHIDI YA SIMBA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here