Yanga Tunisia
Habari za michezo

BAADA YA KUFUNGWA NA WATUNISIA….KIGOGO YANGA ASHINDWA KUJIZUIA…KAFUNGUKA YA NDANI…

admin February 14, 2023 9:57 pm

Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Haji amesema kupoteza kwao dhidi ya US Monastir kwa mabao 2-0 hakujawaondolea malengo yao ya kutinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Arafat amesema matokeo hayo wanayapokea kama njia ya kujipanga kwa uimara zaidi kabla ya kukutana na TP Mazembe Jumapili Februari 19 nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Amesema uongozi wao upo makini kuzipa uzito mechi zote 6 za hatua ya makundi na kwamba kikosi chao kitarudi imara watakapokutana dhidi ya Mazembe.

“Uzuri wa hizi mechi sio kama zile za mtoano, hapa unatakiwa kujipanga utachukuwaje pointi zako kwa ujumla wake ndani ya mechi sita utakazocheza ambazo tatu zipo nyumbani na tatu ugenini,” amesema Arafat.

“Mashabiki wetu wasijiondoe kwenye malengo yetu uongozi wao na timu yao tuko makini watambue kwamba kuna timu iliwahi kufungwa mechi tatu kati ya sita ikaruhusu zaidi ya mabao kumi lakini bado wakafuzu hatua inayofuata.

“Makocha wetu wanajua wapi tumekosea wachezaji wanajua wapi walikosea wanarudi kambini kujiandaa kwa uzito wake dhidi ya Mazembe ninachowaomba mashabiki wetu wasihadaike na kelele zozote wajipange kuja kuipa nguvu timu yao Jumapili Uwanja wa Mkapa,”

JAMAA KAPIGA MIL 20 ZA MERIDIANBET KWA BUKU TANO TU….ONA ALICHOKIFANYA SASA… HII HAPA SABABU YA GEORGE MPOLE KUBAKI SEBULENI CONGO WAKATI TIMU YAKE IKICHEZA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply