Home Habari za michezo MBALI NA MORRISON …HAWA HAPA WACHEZAJI WENGINE WATATU WATAKAO KOSEKANA SIMBA…..

MBALI NA MORRISON …HAWA HAPA WACHEZAJI WENGINE WATATU WATAKAO KOSEKANA SIMBA…..


Simba SC wanakipiga na Pamba FC katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Katika mchezo huo itawakosa Clatous Chama, Sadio Kanoute, Taddeo Lwanga ambao ni majeruhi pamoja na Bernard Morrison ambaye ameagwa na timu hiyo.

Simba itakuwa ikisaka taji la tatu mfululizo la mashindano hayo baada ya kufanya hivyo msimu uliopita na ule wa 2019/2020 na kihistoria ndio timu iliyotwaa ubingwa wa mashindano hayo mara nyingi tangu yaliporudishwa upya msimu wa 2015/2016.

Na endapo itaibuka na ushindi dhidi ya Pamba leo hii, itakutana na Yanga SC kwenye mechi ya nusu fainali ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa katika soka la bongo.

SOMA NA HII  NAMUNGO KAMILI KUMALIZANA NA WAANGOLA LEO KIMATAIFA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here