Home Habari za michezo MECHI NNE BILA GOLI HATA LA KUOTEA….MAYELE AVUNJA UKIMYA..AANIKA VITA ANAYOPITIA LIGI...

MECHI NNE BILA GOLI HATA LA KUOTEA….MAYELE AVUNJA UKIMYA..AANIKA VITA ANAYOPITIA LIGI KUU…


Fiston Mayele; ni staika na mfungaji kinara wa Klabu ya Yanga ambaye anakiri kuwa, mabeki wengi wa Ligi Kuu Bara wamekuwa wakimkamia asifunge kwani hawataki ateteme.

Mayele amesema hayo baada ya mechi dhidi ya Dodoma Jiji ikiwa ni takriban mechi nne hajafunga bao lolote kwenye Ligi Kuu.

Pia amewataka mashabiki wa Yanga kutulia kwani mabao yatakuja na hii ni kama changamoto ya mpira huku akisema muhimu ni malengo ya timu kuchukua ubingwa.

Mechi ya jana dhidi ya Dodoma Jiji ni mechi ya nne kwa mshambuliaji huyo kinara ndani ya Yanga kushindwa kuziona nyazu, ambapo alianza ukame huo kwenye mechi dhidi ya Simba SC.

SOMA NA HII  DILI LA MAKUSU KUTUA SIMBA LAFIKIA PATAMU...VIFAA VINGINE HIVI HAPA ....

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here