Habari za michezo

MOSES PHIRI AWAAGA WACHEZAJI WENZAKE ZAMBIA…MENEJA WAKE AFUNGUKA TIMU ATAKAYOICHEZEA TZ…

admin May 16, 2022 2:48 am


MSHAMBULIAJI wa Zanaco FC ya nchini Zambia, Moses Phiri, rasmi ameaga ndani ya timu hiyo mara baada ya kumalizika kwa msimu huu wa Ligi Kuu ya Zambia.

Phiri ambaye anawindwa na timu za Simba na Yanga, amekuwa katika kiwango bora ndani ya timu hiyo jambo ambalo limepelekea timu hizo kumuwania vikali.

Akizungumza moja kwa moja kutoka nchini Zambia, meneja wa mchezaji huyo, Nyambe Nawa, alisema msimu ujao kuna asilimia kubwa kwa Phiri kucheza Tanzania baada ya kuhitajika na timu za Simba na Yanga.

“Simba na Yanga zote zinamuhitaji Phiri, hivyo mpaka sasa kuna asilimia kubwa sana kwake kucheza soka Tanzania msimu ujao, dirisha la usajili likifunguliwa kila kitu kitakuwa wazi,” alisema meneja huyo.

BAADA YA MORRISON ‘KUFYEKWA SIMBA KIJANJA’…HAWA HAPA MASTAA WENGINE 15 HUENDA NAO WAKAFYEKWA… ZA NDANII KABISAA….PABLO CHANZO CHA MORRISON KUTEMWA SIMBA…ALIMFUKUZA MCHANA KWEUPEE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply