Home Habari za michezo SAA CHACHE KABLA YA MECHI YA LEO…’GUNDU LA SIMBA’ LAZIDI KUMUUMIZA MANARA…AWALILIA...

SAA CHACHE KABLA YA MECHI YA LEO…’GUNDU LA SIMBA’ LAZIDI KUMUUMIZA MANARA…AWALILIA WACHEZAJI…


Msemaji wa klabu ya Young Africans Haji Manara amewahimiza wachezaji wa klabu hiyo kupambana kwenye mchezo wa leo Jumatatu (Mei 09), dhidi ya Tanzania Prisons.

Katika mchezo huo Young Africans watakuwa wenyeji wa Maafande hao wa Jeshi la Magereza kutoka jijini Mbeya ambao wanahaha kujinusuru kushuka daraja msimu huu 2021/22.

Haji Manara ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwahimiza wachezaji wa Young Africans, kwa kuandika ujumbe ambao unasisitiza upatikanaji wa alama tatu katika mchezo wa leo,Itakumbukwa Yanga walitiwa gundu la sare na Simba Juzi, kwenye mechi ya dabi ya kariakoo, ambapo gundu hilo liliendelea kwenye mechi na Ruvu Shooting.

Haji Manara ameandika: Wananchi leo tunahitaji Three Points Only, hakuna Excuse tena, tupo nyumbani katika Uwanja tuliouzoea na tukiwa kamili bila Majeruhi.

Wachezaji wetu tunawaamini na tunawajua uwezo wenu, Yes, Prisons ni Team imara lakini cc ni Team bora mno katika ligi kuu hii.

Nendeni mkawape amani na furaha Wananchi, nendeni mkacheze Soka lenu bila Presha,but tunahitaji Results sahihi jioni ya leo.

Ubingwa wetu upo this May, Uwezo huo mnao na tunajua mtashinda Insha’Allah.

SOMA NA HII  RAIS SAMIA UWANJA WA MKAPA KUSHUHUDIA SIMBA V YANGA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here