Home Uncategorized KURASINI HEATS MABINGWA KIKAPU TANZANIA

KURASINI HEATS MABINGWA KIKAPU TANZANIA


TIMU ya Kurasini Heats imetwaa taji la ubingwa wa kikapu Tanzania (National Basketball League – NBL 2020) kwa kuifunga Oilers 76-59.


 Nafasi ya mshindi wa tatu imeenda kwa Don Bosco Panthers ya Dodoma kwa kuifunga Vijana Basketball Club ya Dar es Salaam 80-77.


Kwa upande wa Wanawake, JKT imetwaa Ubingwa huo na mshindi wa pili ni Don Bosco Lioness zote za Dar es Salaam.


Bingwa wa NBL, Wanaume atawakilisha Tanzania katika mashindano ya kombe la klabu bingwa ya Afrika (Basketball Africa League – BAL) na mshindi wa pili na wa tatu watawakilisha katika mashindano ya vilabu ya kanda ya tano ya Afrika (Zone V Club Championship /Challenge Cup).


 Kwa upande wa wanawake bingwa na mshindi wa pili wote watawakilisha katika mashindano ya vilabu ya wanawake ya kanda ya tano ya Afrika.


Msimu wa Ligi ya Vilabu ya Kikapu ya Tanzania ( NBL) ilianza mwezi Februari mwaka huu kwa ngazi za mikoa (RBA) na imemalizika rasmi leo Oktoba 25, 2020 kwa ngazi ya Taifa.


Kwa sasa uongozi wa kikapu Dar baada ya kumaliza mashindani haya unaingia kwenye maandalizi ya CRDB Bank Taifa Cup 2020, mashindano ya kombe la Taifa yanakayoshirikisha timu za mikoa yanayotarajiwa kufanyika 12-21 Novemba, 2020 Dodoma.



SOMA NA HII  KOCHA HUYU YANGA ANASUBIRI TIKETI ATUE BONGO