Home Habari za michezo UBINGWA EPL NI ZAIDI YA KUPIGA NGUMI CHUMA…KLOPP AIVIZIA MAN CITY…MECHI ZOTE...

UBINGWA EPL NI ZAIDI YA KUPIGA NGUMI CHUMA…KLOPP AIVIZIA MAN CITY…MECHI ZOTE NDANI YA DStv….


Ubingwa wa ligi kuu ya England EPL sasa utalazimika kusubiri hadi siku ya jumapili katika michezo ya mwisho ya kuhitimisha ligi hiyo, baada ya klabu ya Liverpool kupata ushindi wa mgaoli 2 kwa 1 dhidi ya Southampton usiku wa jana katika dimba la St. Marys.

Liverpool sasa imefikisha alama 89 ikiwa nyuma kwa tofauti ya alama 1 na vinara Manchester City wenye alama 90. Baada ya mchezo huo kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuipiku Manchester City kwenye mchezo wa mwisho sio jambo rahisi lakini kwenye football inawezekana.

Ligi kuu ya England itafikia tamati jumapili hii ambapo Manchester City watamaliza ligi dhidi ya Aston Villa katika dimba la Etihad, wakati Liverpool wakimaliza nyumbani Anfield dhidi ya Wolves.

SOMA NA HII  FT: AZAM FC 1-1 SIMBA SC....BOCCO KAWAOKOA TENA..MATUMAINI YA SIMBA YAZIDI KUYEYUKA...YANGA WANATAKA TISA TU...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here