Home Habari za michezo WAKATI INONGA AKIPEWA TUZO YAKE LEO…AHMED ALLY ASHTUSHWA NA ‘SAPRAIZI’ YA MAMILIONI…

WAKATI INONGA AKIPEWA TUZO YAKE LEO…AHMED ALLY ASHTUSHWA NA ‘SAPRAIZI’ YA MAMILIONI…


Beki wa kati wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Henock Inonga Baka amekabidhiwa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa klabu hiyo leo Ijumaa (Mei 06), jijini Dar es salaam.

Inonga alitangazwa kuwa mshindi wa Tuzo hiyo kwa mwezi April 2022, juzi Jumatano (Mei 04), baada ya kuwashinda wachezaji wenzake Shomari Kapombe na Joash Onyango.

Beki huyo kutoka DR Congo amekabidhiwa Tuzo hiyo katika ofisi za Emirate Aluminium Profile wanaodhamini Tuzo hizo ndani ya klabu ya Simba SC.

Wakati huo huo Kampuni ya Emirate Aluminium Profile imemzawadia Tuzo Binafsi Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally sambamba na Shilingi Milioni Mbili, kuafutia kazi kubwa aliyoifanya tangu alipokabidhiwa jukumu la kuisemea klabu hiyo.

 Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo Issa Maeda amesema: “Hii ni tuzo maalum na haina mchakato wa kupigiwa kura, Kampuni ya Emirate Aluminium Profile imeamua kumzawadia Ahmed Ally baada ya kuupiga Mwingi.”

Naye Ahmed Ally ametoa nano lake la kushukuru kwa Uongozi wa Kampuni ya Emirate Aluminium Profile kwa kusema: “Niushukuru sana Uongozi wa kampuni hii kwa Suprize hii kubwa ambayo kiukweli inashtua na inafurahisha.”

“Hawakuniambia wala hawakumwambia mtu yoyote kuna zawadi kubwa wameniandalia, nilikuja hapa kushuhudia na kushiriki zoezi la kumkabidhi Tuzo beki wetu Henock Inonga Baka, nikakutana na zawadi yangu.”

SOMA NA HII  KISA MGUNDA...JULIO AWASHUKIA MABOSI WA SIMBA....AFUNGUKA KUHUSU NAFASI YA MBRAZILI...