Home news HIVI NDIVYO SIMBA WALIVYOYEYUSHA DAK 339 KUTAFUTA GOLI MOJA KWENYE LIGI KUU..HALI...

HIVI NDIVYO SIMBA WALIVYOYEYUSHA DAK 339 KUTAFUTA GOLI MOJA KWENYE LIGI KUU..HALI NGUMU…


Klabu ya Simba imerudisha heshima yake iliyopotea kwenye takribani michezo mitatu ya Ligi Kuu ya NBC baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mbeya City, Mtibwa Sugar na Kagera Sugar ndio waliopoteza matumaini ya WanaSimba baada ya kuwazuia kutopata hata bao hata moja katika michezo yao mitatu ya ligi ambayo walifungwa mara mbili na kutoa sare moja.

Wekundu wa Msimbazi wametumia takribani dakika 339 kupata bao ambapo dakika ya 69 ya mchezo dhidi ya Prisons ilipata mkwaju wa penalti uliowekwa kimiyani na mshambuliaji  Meddie Kagere.

Penalti hiyo ilileta sintofahamu kwa mashabiki uwanjani hapo kutokana na mazingira tata yaliyojitokeza hadi kupatika na kwakwe ambayo Kagere aliitumia vizuri kujiandikia bao lake la tano msimu huu.

Kipindi cha pili Simba ilifanya mabadiliko ya kumtoa Mzamiru Yassin na nafasi yake ikichukuliwa na Pape Ousmane Sakho Ili kuongeza nguvu zaidi kwenye mashambulizi.

Mabadiliko hayo yalionekana kuleta tija kwani Simba ilionekana kushambulia zaidi kutafuta bao la utangulizi huku Prisons wakiendelea kutumia mbinu zile zile za kipindi cha kwanza za kujilinda.

Kwa upande wa Prisons ilimtoa Lambert Sabiyanka huku nafasi yake ikichukuliwa na Mohamed Mkopi Ili kuongezea nguvu eneo la ushambuliaji ambalo kwa kipindi cha kwanza lilionekana kutokuwa na madhara makubwa kwa safu ya ulinzi ya Simba inayoongozwa na mabeki Joash Onyango na Henock Inonga.

Huu ni mchezo wa 14, kwa Kila timu ambapo Simba imeshinda michezo nane, sare nne na kupoteza miwili, wakati Tanzania Prisons imeshinda mitatu, sare mbili na kupoteza tisa.

Matokeo haya yanaifanya Simba kuibuka na ushindi wake wa kwanza dhidi ya Tanzania Prisons tangu iliposhinda mara ya mwisho bao 1-0, Mei 5, 2019.

Ushindi kwa Simba unaifanya kufikisha pointi 28, nyuma ya pointi saba kutoka kwa Yanga yenye pointi 35, ambayo itacheza Jumamosi hii katika Uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Mbeya City.

SOMA NA HII  CHAMA: SIMBA WANAWEZA KUZIBA PENGO LANGU....

Kwa upande wa Tanzania Prisons inaendelea kusalia mkiani mwa msimamo na pointi 11.