Home Habari za michezo BAADA YA KUTAKATA CHINI YA NABI….’BACCA’ KAANGALIA UPEPO WA MSIMU UJAO YANGA..KISHA...

BAADA YA KUTAKATA CHINI YA NABI….’BACCA’ KAANGALIA UPEPO WA MSIMU UJAO YANGA..KISHA AKASEMA HAYA…

Habari za Yanga SC

Beki wa Yanga, Ibrahim Bacca alikuwa na msimu mzuri ndani ya Yanga, baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Nasreddine Nabi kumtengeneza awe mchezaji wa kuaminika, jambo alilokiri limempa ujasiri wa kuhakikisha anakiendeleza kiwango chake, akiahidi kurudi na moto zaidi msimu ujao.

Bacca alisema licha ya kutajwa midomo mwa mashabiki mara kwa mara, kwake anachukulia kama alamu ya kulinda kiwango chake, kwani anatambua wanapenda kazi anayofanya na siyo jambo lingine, hivyo hawezi kutoka nje ya mstari wa kujituma kwa bidii na kujilinda zaidi.

“Nimepata nafasi ya kucheza na kuonekana lazima nilinda kiwango, kwani soka ni kazi, siwezi kulewa sifa na kujiona nimefika wakati bado nina safari ndefu ya kufanya vitu vingi kwenye karia yangu.

“Naamini mashabiki wanapenda kuona unainufaisha klabu yao, hivyo siwezi kujisahau na kuona nimekuwa staa, badala yake natamani huduma yangu iendelee mbele na siyo kurudi nyuma, jambo ambalo hata baba yangu ananisisitiza sana kutunza nidhamu ya kazi.”

Alisema anajua karaha ya kusugua benchi na raha ya kupata nafasi ya kucheza, kwani Yanga hakuanza moja kwa moja kikosi cha kwanza, alisubili hadi zamu yake ilipomfikia, jambo linalomfanya azingatie miiko ya soka inataka nini.

“Kama ni benchi nimekaa ndio maana nasisitiza kwamba natamani kupambana zaidi ya msimu ulioisha ambao kwangu ulikuwa mzuri, kikubwa ni kuomba uzima na afya njema,” alisema.

SOMA NA HII  ILE ISHU YA MSUVA KUTAKIWA NA TP MAZEMBE KUMBE IKO HIVI AISEE...WENYEWE WAFUNGUKA KILA KITU...