Home Habari za michezo JEZI MPYA SIMBA NI KESHO….BEI YATAJWA MAPEMAAA…

JEZI MPYA SIMBA NI KESHO….BEI YATAJWA MAPEMAAA…

Jezi Mpya za Simba Kimataifa

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amewataka mashabiki na wanachama wa Simba kujiandaa kikamilifu kununua jezi mpya kwani mzigo unatua nchini kabla ya sikukuu ya Idd, Juni 29, 2023.

Akizungumza kupitia Simba APP, Ahmed amesema anafahamu mashabiki wana shauku kubwa ya kuvaa ‘uzi’ mpya hivyo wasiwe na mashaka kwani unaingia kabla ya sikukuu ya Idd inayotarajiwa kusherehekewa kesho  Aalhamisi.

“Mzigo ni mwingi na wa kutosha. Niwaambie tu mashabiki wajiandae na shilingi elfu thelathini na tano zao, mzigo utakuwa wa kutosha hata kama mtu atataka awe na jezi kumi peke yake,” alisema Ahmed.

Ahmed alisema, baada ya kuingia nchini, taratibu za kuuingiza sokoni zitafanyika na maduka yote yatakuwa na mzigo kwa wakati mmoja.

SOMA NA HII  PATRICK AUSSEMS AKIMBIA TIMU KENYA....AISHIA KUWAPA MATUMAINI KWA 'VIDEO CALL'...TIMU YA RWANDA YATAJWA KUHUSIKA...