Home Azam FC BAADA YA KUZIPUNA SIMBA NA YANGA….ISHU NA MORRISON NA AZAM FC IKO...

BAADA YA KUZIPUNA SIMBA NA YANGA….ISHU NA MORRISON NA AZAM FC IKO HIVI…

Tetesi za Usajili Bongo

Imekuwa ikitajwa kuwa mabosi wa Azam FC wapo kwenye mpango wa kuinasa saini ya Bernard Morrison.

BM aliyekuwa kiungo wa Yanga raia wa Ghana kwa sasa yupo huru jambo lililowafanya viongozi wa klabu hiyo kuibuka na kuweka wazi kuwa nyota huyo hayuko kwenye mipango yao.

Morrison alitangazwa kutokuwa kwenye mipango ya Yanga kwa msimu ujao usiku wa kuamkia Alhamisi, mara baada ya kumaliza mkataba wake ndani ya timu hiyo.

Baada ya kuachwa huko kukawa na tetesi za Mghana huyo kuhusishwa kujiunga na timu za Singida Fountain Gate na Azam FC baada ya Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Abdulkarim Amin ‘Popat’ kunaswa akizungumza naye mara baada ya mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports iliyopigwa Mkwakwani jijini Tanga.

Akizungumzia uwezekano wa Morrison kukipiga ndani ya Azam, Popat alisema:

“Kuhusiana na mazungumzo yangu na Morrison mara baada ya mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports yalikuwa ya kawaida kwa kuwa sisi ni watu wa mpira na tulikuwa tunapeana pole ya mchezo.

“Hivyo hatukuzungumza suala lolote linalohusu usajili na kwa ujumla hatuna mpango wa kumjumuisha kwenye kikosi chetu kwa msimu ujao.”

SOMA NA HII  MOSES PHIRI AENDELEA KUZICHEZESHA REDE SIMBA NA YANGA....AFUNGUKA MUSTAKABALI WAKE NA ZANACO...