Home Uncategorized SHIKALA MBABE WA LUIS NA SADALLA, ASEPA NA TUZO YA BAO BORA

SHIKALA MBABE WA LUIS NA SADALLA, ASEPA NA TUZO YA BAO BORA

 PASTON Shikala, nyota wa Mbeya City ameibuka mshindi wa tuzo ya bao bora kwa msimu wa 2019/20.


Bao la Shikala lilipatikana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara walipomenyana na JKT Tanzania.


Amewapoteza washindani wenzake ambao ni Luis Miqussone wa Simba aliyefunga bao mbele ya Alliance FC na Sadallah Lipangile wa KMC aliyefunga bao mbele ya Mtibwa Sugar.


Pia Sunday Manara amepewa tuzo ya heshima kwa msimu wa 2019/20 kwenye kilele cha tuzo ndani ya Ukumbi wa Mlimani City.

SOMA NA HII  YANGA YATOA RAMANI NZIMA YA KUSEPA NA UBINGWA WA LIGI KUU BARA