Home Habari za michezo WAKATI LIVERPOO WAKIMTAKA SON KAMA MBADALA WA MANE….ARSENAL WAJICHOMOZA KUTIKISA KIBERITI….

WAKATI LIVERPOO WAKIMTAKA SON KAMA MBADALA WA MANE….ARSENAL WAJICHOMOZA KUTIKISA KIBERITI….


JURGEN Klopp alipanga kupeleka ofa ya kumnasa Son Heung-min kwenye dirisha la majira ya kiangazi la mwaka huu akakipigeLiverpool, lakini Arsenal imetibua mpango wote kwa mujibu wa football.london.

Son ni moja ya washambuliaji matata kabisa kwenye Ligi Kuu England akiwa na uwezo wa kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha timu yoyote huko Ulaya. Na sasa wakati Sadio Mane anajiandaa kuachana na Liverpool kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi, Son alipangwa na kocha Klopp kuwa mbadala sahihi huko Anfield.

Na Liverpool ikiingiwa na hofu ya kumpoteza mmoja kati ya Mane na Mohamed Salah, waliandaa mkwanja wa kutosha kwa ajili ya kwenda kunasa huduma ya mkali huyo wa Korea Kusini. Liverpool iliamini kwamba Tottenham isingenasa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, jambo ambalo lingewapa urahisi kwenye kumnasa Son, lakini Arsenal imetibua baada ya kuenguliwa kwenye Top Four na Spurs kucheza Ulaya msimu ujao.

Klopp amekuwa shabiki wa Son kwa muda mrefu, ambapo staa huyo wa Korea alianza kutengeneza jina lake kwenye soka tangu alipokuwa Borussia Dortmund. Klopp na Son walionekana wakizungumza wakati Liverpool ilipocheza na Tottenham.

Na Liverpool ilikuwa imejiandaa kumchukua Son, lakini Spurs chini ya kocha Antonio Conte imekuwa moto na kuiengua Arsenal kwenye mchakamchaka wa Ligi ya Mabingwa Ulaya jambo ambalo litawafanya wasipoteze wakali wake muhimu akiwamo straika, Harry Kane.

SOMA NA HII  MBAPPE AFICHUA ALIVYOITOSA LIVERPOOL....PAMOJA NA MAMA YAKE KUINGILIA KATI LAKINI WALITOKA 'KAPA'....