Home Habari za michezo WAKATI WADAU WAKIMTILIA SHAKA KUHUSU KIMO CHAKE KAMA BEKI…DICKSON JOB AIBUKA NA...

WAKATI WADAU WAKIMTILIA SHAKA KUHUSU KIMO CHAKE KAMA BEKI…DICKSON JOB AIBUKA NA KUWAJIBU HAYA…


Beki Dickson Job wa Yanga amesema hayupo tayari kuona timu yake inapoteza kwa sasa kwa sababu lengo lao ni kumaliza Ligi bila kufungwa.

Yanga mpaka sasa wamecheza mechi 21 bila kupoteza na kuifanya iwe timu pekee ambayo haijafungwa kwenye Ligi.

Akizungumza Job alisema;

“Kikubwa mpaka sasa kwanza atuhitaji kupoteza mchezo wowote na ili tusipoteze tunahitaji kucheza mechi bila kuruhusu goli kwa kila mchezo, sisi kama walinzi wa timu tupo tayari kwa ajili ya kupambana ili kutimiza malengo yetu.”

Job aliongeza kuwa;

“Mimi na Mwamnyeto tuna maelewano makubwa na kucheza kwetu muda mrefu tunajuana vizuri na ndio maana kila mmoja anatoa kile anachostahili kwa wakati.”

Job amejiunga na Yanga kwenye msimu dirisha dogo la msimu uliopita na tangu ameingia kwenye kikosi cha Nasreddine Nabi amejihakikishia nafasi akicheza sambamba na Bakari Mwamnyeto.

Awali mashabiki wa Yanga walikuwa na wasiwasi na kimo cha Job.

SOMA NA HII  BAADA YA KUFUNGWA NA WATUNISIA....KIGOGO YANGA ASHINDWA KUJIZUIA...KAFUNGUKA YA NDANI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here