Home Habari za michezo WALICHOFANYA INONGA NA MAYELE KWA MASHABIKI WA YANGA JUZI…KILA MMOJA ALIWAINUA KUSHANGILIA..

WALICHOFANYA INONGA NA MAYELE KWA MASHABIKI WA YANGA JUZI…KILA MMOJA ALIWAINUA KUSHANGILIA..


Muda mfupi kabla ya mechi kuanza beki wa kati wa Simba, Inonga Baka aliingia uwanjani na kwenda upande waliokuwa wachezaji wa Yanga (Kaskazini) kuwainua mashabiki wao na kutaka kumshangilia pamoja na timu yake.  

Inonga hakuonekana wakati timu zimepanga mistari kutoka vyumbani kuingia uwanjani na hata muda wa kusalimiana pamoja na waamuzi hakuwepo.

Wakati timu zilikuwa kwenye maeneo ya kupiga picha na kusubiri nanahodha kuchagua magoli ndio Inonga aliingia Uwanjani.

Baada ya kuingia alienda upande waliokuwa wachezaji wa Yanga na kuwainua mashabiki wao kwa kuonyesha inshara za kuwashangilia.

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele nae wala hakuonyesha upole kwani muda huo huo aliwainua mashabiki wa Yanga kwa kutaka washangilie kama vile alivyofanya Inonga.

SOMA NA HII  PABLO AAMUA LIWALO NA LIWE SIMBA...AWAPIGA CHINI SHIBOUB NA MOUKORO...'TRY AGAIN' ATOA KAULI...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here